Mbunge wa Mbeya mjini,Joseph Mbilinyi 'Sugu' ametoa ufafanuzi wa kwanini wananchi wa Mbeya
walimpa jina la 'Rais wa Mbeya'.
Sugu akiongea na Azam TV amesema jina hilo limetokana na kile alichodai ni kufanya mambo mengi kwa wananchi hao ambayo awali yalishindikana.
"Nilipokuja mimi nakuleta suluhisho kwa kushirikiana na wananchi, wenyewe wahakaona huyo tumuite Rais wetu, sio kitu kibaya,
"Kwa hiyo haikuwa sasa, Sugu kasema sasa niite Rais, no!, ni wananchi wengine," amesema Sugu.
Kauli ya Sugu inakuja mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kupiga marufuku Mbunge kujiita Rais na kudai kuwa kila mmoja asimamie nafasi yake na majukumu yake.