Tamko la TRA kwa wanaoweka matangazo kwenye magari
0
February 03, 2019
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeeleza juu ya uwepo wa ulazima wa ulipaji kodi kwa watumiaji wa vyombo va usafiri nchini ambao wamekuwa wakiweka matangazo kwenye magari ambapo wamekuwa wakitembea maeneo mbalimbali ya nchi.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema “kuna mabango ya kawaida yamesimikwa, mabango yaliyo juu ya majengo na mabango ya kwenye magari ambayo gari kila likizunguka linakuwa na bango hilo, mfano kampuni za vinywaji, biashara ya bidhaa mbalimbali,”.
Aidha kuhusiana na kodi hiyo Kayombo amesema kuwa “sio kodi mpya na si kitu cha ajabu, magari haya yanastahili kulipiwa, kwa mfano bango lipo katika gari linazunguka nchi nzima linaonwa na watu wengi zaidi kuliko bango lililowekwa sehemu moja.”
Hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kulianza kusambaa barua ikimnukuu meneja wa kodi wa mamlaka ya mapato TRA ikimtamka moja ya wafanyabiashara wilayani humo kulipa kodi ya tangazo kupitia moja ya magari yake.
Tags