Tatizo la Simba Lipo Wapi?
0
February 03, 2019
Napenda kuwapa hongera Al Ahly, kwa kutumia uwanja wake wa nyumbani, kwa kumfunga Muwakilishi wetu kutoka Tanzania, Simba, kwa mabao 5-0 katika michuano ya klabu Bingwa Barani Afrika.Simba,wamepoteza michezo miwili kwa idadi kubwa ya mabao 10-0 yote ni mchezo ya ugenini hii inatoa taswira kuwa Simba, bado ajajua umuhimu wa kuchezea mechi katika viwanja vya ugenini.
Turudi katika mchezo wa leo dhidi ya Al Ahly, Simba kwenye mchezo huu walianza kwa presha kubwa sana kwa kulishambulia lango la Al Ahly, kumbe wapinzani wao walikuwa wanajaribu kuwasoma mbinu zao.Simba, bado kuna mapungufu makubwa katika idara ya ulinzi ukiongozwa na Pascal Wawa, na Juuko Murshid, wamekuwa hawana ushirikiano mzuri ni wazuri wakiwa na mpira pale wanapokutana na washambuliaji wajanja wenye uwezo wa kulazimisha kufanya makosa na kuzitumia nafasi.
Ukiangalia magoli yote waliyofungwa leo ndani ya boksi lao na hayana migogoro jinsi gani katika idara hiyo imekuwa aina umakini.Simba, wanahitaji waingie sokoni wafanye usajili katika idara hiyo wapate mabeki wa kati wenye uwezo mkubwa wa kushambulia na kukaba ukiangalia vizuri timu zote ambazo Simba, amefungwa wapo vizuri katika idara ya ulinzi na wana nidhamu ya kimchezo.Mwalimu Patrick Aussems, sina elimu ya kumzidi kwa sababu amesomea ukocha na leseni ya ngazi hiyo ya daraja la juu.Pengine mpaka leo ajagundua makosa ya timu yake timu zote alizocheza nao muda mwingi walikuwa wakitengeneza nafasi kwa mashambulizi ya pembeni, ukirudia kwenye mchezo dhidi ya JS Saoura japo walishinda ilikuwa ngumu kugundua kuwa JS Saoura, walikuwa wakishambulia kutokea wapi? me naamini kocha wa Al Ahly, alikaa chini ya kurudia mkanda wa As Vita, dhidi ya Simba,na kugundua madhaifu hayo.Simba ,inahitaji ijitafakari kwenye michezo iliyobakia kama wataweza kumzuia Al Ahly, mchezo wa marudiano kwa kumdhibiti asishambulie kutokea pembeni na kumfanya acheze mpira katika idara ya Kiungo wanaweza kupata matokeo.Mkude, na Kotei, bado walishindwa kufanya kazi ambayo wamepewa na mwalimu kwa sababu Al Ahly, walikuwa hawakai na mpira sana katika idara ya Kiungo, walikuwa ni wazuri kwenye kupeleka mpira pembeni.Azizi _Mtambo 15