Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ally Mchungahela ameeleza kuwa tayari wameshakutana na Viongozi wa Yanga kumalizana na sasa kinachosubiriwa ni kutangazwa kwa tarehe nyingine.
Ikumbukwe kuwa uchaguzi huo ulipaswa kufanyika Januari 13 mwaka huu lakini kutokana na baadhi ya wanachama kufungua kesi Mahakamani kusimamisha mchakato huo ilipelekea pia zoezi la uchaguzi kusimama.
"Uchaguzi wa Yanga utafanyika, hakutakuwa tena na mchakato mwingine mpya bali utaendelea palepale ulipokuwa umefikia, tarehe 5 Machi tutatangaza rasmi tarehe mpya ya uchaguzi wa Yanga na naamini utafanyika" alisema.
Mchungahela ameeleza kuwa anaamini mpaka kufikia siku hiyo kila kitu kitakuwa sawa na hakuna kizuizi kingine ambacho kitafanya mchakato huo usimame.