Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Tanzania T.I.D a.k.a TOP a.k.a Warioba A.k.A BASATA a.k.a POWER BANK leo kupitia instagram yake amwaga povu kali kiwango cha grisi kutoka kwa Azam TV baada ya kurusha filamu yake ya Girlfriend bila ya kibali maalumu.
Maneno yake yanasomeka kama ifuatavyo:
"Tangazo Tangazo.......Ni Marukufu kwa Azam TV Kuonyesha Filamu ya Girlfriend popote pale bila kunilipa Haki zangu,Sioni Sababu ya kuendelea Kuibiwa Haki Zangu,Nawadai Milioni mia (300) kwa kurusha Filamu hii bila Kunilipa wala Makubaliano ....I hate this kwanini Hamnilipi Haki Zangu!!!"
TID Awapa Onyo Azam TV kucheza Filamu yake ya Girlfriend. Awadai Millioni 300 Kwa Kukaidi
0
February 24, 2019
Tags