Tundu Lissu ahojiwa kuichafua Tanzania

Tundu Lissu ahojiwa kuichafua Tanzania
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema kuwa kuwa serikali haina hoja ya msingi juu ya kutofanyika kwa uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwake mnamo Septemba 2017 alipokuwa Bungeni Jijini Dodoma.

Akizungumza kwenye mjadala juu ya uhuru wa kujieleza katika kituo cha kimataifa cha Sauti ya Amerika (VOA) ambapo ilishuhudia pia ushiriki wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi ambapo mbali na mambo mengi Lissu alihojiwa juu ya kuichafua Tanzania kupitia ziara yake anayoifanya.

Akihoji juu ya ziara yake nje nchi, Balozi wa Tanzania wa nchini Marekani amesema, “kitendo cha Lissu kuzunguka dunia nzima hakisaidii,  BBC, Radio Ujerumani -DW, Sauti ya Amerika -VOA, sio mahakama, unachofanya ni kutuchafua na kutuvunjia heshima na kujichafua wewe mwenyewe”.

Akijibu madai hayo Mbunge wa Singida Mashariki juu ya kuichafua Tanzania Lissu amesema, “lazima tutafautishe kati ya serikali na taifa, serikali ya Magufuli sio taifa serikali inatakiwa kuongozwa na Katiba, na Katiba yetu imeweka wazi mipaka ya mamlaka sisi raia".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad