Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu leo anafanyiwa upasuaji wa 23 na wa mwisho katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg nchini Ubelgiji.
Lissu amesema baada ya upasuaji huo utakaofanywa kwenye goti la mguu wake wa kulia atakuwa tayari kurejea nyumbani mwaka huu.
Tundu Lissu yupo nje ya nchi tangu Septemba 7 mwaka juzi aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa maeneo ya nyumbani kwake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria Mkutano wa Bunge.