Ubalozi wa Marekani nchini Kenya watoa tahadhari ya Ugaidi
0
February 04, 2019
Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umeonya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa shambulizi la kigaidi dhidi ya raia wa mataifa ya magharibi katika miji ya Nairobi, Naivasha,Nanyuki na ukanda wa pwani ya Kenya.
Hatua hiyo inakuja kufuatia hivi karibuni nchi ya Kenya kutikiswa na shumbalio la kigaidi ambapo watu zaidi ya 20 walifariki.
Utakumbuka mwezi uliopita mamia ya watu walilazimika kutoroka umwagikaji damu ulioshuhudiwa katika hoteli ya DusitD2 na jengo la kibiashara. Kenya imekuwa ikilengwa na kundi la al Shabab tangu Okotoba 2011, wakati taifa hilo lilipotuma vikosi vyake nchini Somalia kupambana na kundi hilo la jihadi.
Tags