Unyama Mtupu: Mwili Wa Mtoto Watelekezwa Kwenye Ndoo Makambako

Unyama Mtupu: Mwili Wa Mtoto Watelekezwa Kwenye Ndoo Makambako
Wanawake mkoani njombe wametakiwa kuacha Tabia ya kutoa ujauzito na kutupa watoto wachanga wasio na hatia kwa kisingizio cha Ugumu wa Maisha kwani kufanya hivyo ni kinyume na matakwa ya Haki za Binadamu.

Hayo yamesemwa na wananchi wa mtaa wa Mangula katika Halmashauri ya Mji wa Makambako  mara baada ya kumkuta mtoto mchanga anayekadiliwa kuwa na miezi saba ambaye amewekwa kwenye ndoo na kutupwa na mama ambaye hajafahamika jina lake mpaka sasa katika eneo la uwanja wa amani mjini makambako.

Aidha mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mangula uliopo kata ya Mji mwema Roina Ngimbuchi amethibitisha kuokotwa kwa mtoto huyo, ambapo amesema kuwa mhusika wa tukio hilo mpaka sasa hajafahamika lakini serikali  inaendelea na upelelezi wa kumbaini mtu ambaye amehusika na tukio hilo  la kinyama linalo kiuka haki za watoto.

Mganga mfawidhi wa hospital ya Makambako Kesha mgunda  amekiri kupokea mwili wa mtoto mchanga na kueleza kuwa mwili huo umehifadhiwa katika hospitali hiyo.

Hata hivyo mganga mfawidhi wa hospitali hiyo amewataka akina mama na wanawake wote kutumia uzazi wa mpango ili kuepukana na mimba zisizo tarajiwa ili kuepuka kufanya matukio yanayohatarisha uhai wa watoto.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad