Urusi Yajitoa Mkataba wa INF, Yatangaza Kuunda Makombora Mapya


Urusi imejiondoa katika mkataba wa kupinga uundaji wa makombora ya masafa marefu uliofikiwa enzi ya vita baridi kufutia uamuzi sawa na huo uliochukuliwa na Marekani.

Rais Vladimir Putin amesema taifa hilo litaanza kuunda makombora mapya.

Marekani ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo ilitangaza kujitoa siku ya Ijumaa.

Mkataba huo uliofikiwa kati ya Marekani na muungano wa Sovieti, USSR na kutiwa saini mwaka 1987 ulipiga marufuku mataifa yote dhidi ya matumizi ya makombora ya masafa mafupi na yale ya kadri.

"Washirika wetu wa Marekani wametangaza kujitoa katika mkataba huo nasi pia tunafuata mkondo wao,"alisema Bw. Putin siku ya Jumamosi.

Katibu mkuu wa muungano wa kijeshi wa mataifa ya magharibi Nato, Jens Stoltenberg amesema: "Washirika wote [Ulaya] wameunga mkono hatua ya Marekani kwasababu Urusi imekiuka mkataba huo kwa miaka kadhaa."

Urusi imekuwa ikikanusha tuhuma za kukiuka mkataba wa vita baridi.

Rais wa Putin aidha amesema tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba huo.

Marekani imesema ina ushahidi kuwa kombora jipya lililoundwa na Urusi ni moja ya mokombora yaliyopigwa marufuku katika mkataba wa INF.

Baadhi ya maafisa wa Marekani wanasema kuwa makombora ya aina ya 9M729 - yanayotambuilwa na Nato kama SSC-8 tayari yameanza kutumika.

Katika mkutano wa Jumamosi akiandamana na mawaziri wake wa ulinzi na wa mambo ya nje, rais Putin alisema wataanza kuunda silaha mpya ikiwa ni pamoja na makombora ya kulipua meli na mengine yaliyo na kasi ya mara tano zaidi ya mlio wasauti.

Bw. Putin hata hivyo amesema kuwa hatajihusisha katika mradi wa gharama ya juu ya uundaji silaha na kuongeza kuwa taifa lake litatumia silaha hizo endapo marekani itaanza kuzitumia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad