USHUHUDA: Japo Nililazimishwa Kuoa, Tena Msichana Walionichagulia Wazazi Ndoa yangu Imekuwa Neema na Baraka Bila Kutegemea
0
February 24, 2019
Imepita mwaka mmoja toka nioe baada ya kulazimishwa sana mpaka mzee kufikia kuniambia "Hakuna chochote nilichowahi kukushauri na ukafanya navotaka,kwahili mwanangu nakuomba uoe utulie sitaki uwe mzinzi na muhuni" Nikajiskia vibaya sana nikaamua bora nioe kuwaridhisha wazazi.
Mwaka umepita sijategemea kama ndoa yangu ingekua tamu hivi japo mi na mke wangu vitu vingi hatuendani lakini sijawahi kupata mapenzi na wala kupenda kama sasa ivi kuna siku nilisafiri kama wiki hivi narudi mke wangu ananipokea kwa furaha ya machozi na tulimissiana kinyama.
Kiuchumi ndio kwenye miujiza wallah,ndani ya mwaka mmoja tu wa ndoa nimepiga hatua kubwa sana biashara yangu yazidi kukua na mambo yanaenda kusema kweli ungeniuliza miaka miwili iliyopita kama utaoa lini ningekwambia nitaoa nikifika 30,lakini nimeoa na 25 na sijutiii bless you all
Ushuhuda: Japo Nililazimishwa Kuoa, Tena Msichana Walionichagulia Wazazi Ndoa yangu Imekuwa Neema na Baraka Bila Kutegemea
Tags