Vitambulisho vya Rais Magufuli vyamponza Sugu

Vitambulisho vya Rais Magufuli vyamponza Sugu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amethibitisha jeshi hilo kumuita Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu kwa kile walichokisema kuwa Mbunge huyo ametoa kauli ya uchochezi.

Kwa mujibu wa Kamanda Matei, zoezi la kugawa vitambulisho lilikuwa na lengo zuri la kuwambua wafanyabiashara hao lakini Mbunge huyo ameonekana kulikosoa kwa kutoa maneno ambayo yaliashiria uchochezi.

Kamanda Matei amesema, "ni kweli tumemuita Mbunge Joseph Mbilinyi kwa mahojiano kutokana na maneno yake aliyoyazungumza kuhusu vitambulisho, maana tunaona kuna kukashifu, vile ni vitambulisho vilivyotolewa na serikali sasa tunapoona mtu anaanza kutoa maneno hayo, huo ni uchochezi"

Mapema wiki hii Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila alibainisha juu ya uwepo wa baadhi ya kauli zilizoashiria kudharau tukio la kugawa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo maarufu.

Disemba 2018 Rais Dkt John Pombe Magufuli aliwakabidhi Wakuu wa Mikoa vitambulisho maalum kwa ajili ya kuvigawa kwa wafanyabiashara wadogo ili waweze kutambulia.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad