Wakazi Atoa ya Moyoni Kifo cha Zilla "Nashukuru Mungu kwa Kumaliza Tofauti Zetu"

Wakazi Atoa ya Moyoni Kifo cha Zilla "Nashukuru Mungu kwa Kumaliza Tofauti Zetu"
Baada ya kuaminika kuwepo kwa bifu kati ya Wakazi na Marehemu King Zillah, Wakazi ameweka wazi kwamba anamshukuru Mungu kwa kumalizi tofauti zake na Rapa huyo aliyefariki usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwao.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rapa Wakazi amendika hayo katika salamu zake za pole kwa familia na mashabiki wa Rapa Godzillah ambaye alikuwa akiwakilisha Salasala katika muziki huu wa kizazi kipya.

Licha ya Juni, mwaka 2017, Wakazi na King Zillah kuonekana kama ni mahasimu, Rapa huyu ameeleza kwamba Zillah alikuwa kati ya Marapa bora kwenye stali ya mitindo huru (Free Style).

Wakazi ameandika, "Kweli maisha ni mafupi, umeondoka mapema sana, lakini kama ulivyosema  hata ukifa utaendelea kukumbukwa. Ni kweli. I'm glad we reconciled our differences and misunderstanding before your untimely demise. I pray that the Lord gives your family strength through this tough time. My condolences to your family, friends and fans".

Ameongeza, "No one cared for Salasala until you screamed it. You were one of the best Freestyle Rappers. Nafasi yako kwenye muziki wetu is well cemented. Najua miaka ya karibuni umepitia kipindi kigumu ila always ulibakia kuwa vilevile na hujawahi kumlaumu mtu. Your heart was big enough to carry all that pain. I admired you for that. Asante for the music and the few memories we shared. Rest In Peace Godzilla aka King Zilla (Golden Jacob Mbunda)"\

Hata hivyo katika moja ya mahojiano aliyoyafanya Desemba 2018, Godzila aliweka wazi kuhusu kumaliza ugomvi wake na Rapa Wakazi ambapo alisema yale yalishapita na kwamba ugomvi kwa vijana kama wao ni mambo ya kawaida.

"Wakazi ni mwanangu sana, hayo yalishapita na sasa tumekuwa na kuyaacha yapite na ambacho watu hawajui ni kwamba mimi na Wakazi tunawasiliana sana kwa sababu tuna kundi letu ambalo tunacheza wote baskeball, lakini ugomvi ni mambo ya kawaida. Mkiwa mnafanya kazi pamoja kupishana kauli kupo tu", alisema Godzilla.

Usiku wa kuamkia leo Februari 13, 2018 Rapa Godzillah alifariki dunia na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam ambapo Mtu wake wa karibu ameeleza kuwa presha ilishuka na sukari ilipanda pamoja na kuumwa na tumbo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad