Wakili wa zamani wa Trump aliambia bunge kuwa rais huyo wa Marekani alipanga uongo

Wakili wa zamani wa Trump aliambia bunge kuwa rais huyo wa Marekani alipanga uongo
Wakili wa zamani wa rais wa Marekani Donald Trump, Michael Cohen amedai kwamba kiongozi huyo alimtaka adanganye kuhusu mpango biashara kuhusu biashara ya ujenzi wa jengo mjini Moscow wakati wa kampeni ya uchaguzi wake.

Katika ushahidi alioutoa bungeni, Cohen amesema Trump aliratibu mipango ya siri kwa ujenzi wa jengo kubwa, hata wakati alikana kuhusika na biashara yoyote Urusi.

Ameeleza pia kwamba Trump alifahamu kuhusu kufichuliwa kwa barua pepe zilizodukuliwa za chama cha Democrat na amemuita kiongozi huyo "mbaguzi", "tapeli" na "muongo".

Trump alijibu: "Anadanganya ili kupunguza kifungo chake gerezani."


Rais wa Marekani alichukua muda katika kujitayarisha kukutana na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un huko Hanoi, Vietnam, siku ya Jumatano kumjibu kupitia ujumbe wa Twitter wakili wake huyo wa zamani.

Cohen, mwenye umri wa miaka 52, atatumikia kifungo cha miaka mitatau gerezani kuanzia Mei kwa kukiukasheria ya ufadhili wa kampeni kwa kumlipa mojawapo ya wanaodaiwa kuwa mahawara wa Trump pesa za kumnyamazisha, kukwepa kulipa kodi na kulidanganya bunge.


Katika ushahidi wake wa wazi katika kamati ya bunge la wawakilishi Jumatano, amesema Trump "alifahamu na aliratibu" mipango ya ujenzi wa jengo 'Trump Tower' mjini Moscow, huku akikiri wazi kwamba hana biashara yoyote na Urusi.

"Wakati huo huo nilikuwa nashauriana na kujadiliana na Urusi kwa niaba yake," Cohen ameeleza katika ushahidi wake, "angeniangalia machoni na aniambie hakuna bishara yoyote Urusi na alafu atoke aende kuwadanganya raia wa Marekani kwa kusema hilo hilo. Kwanamna yake, alikuwa akiniambia nidanganye.."

"Alitaka nidanganye," aliongeza.

FBI 'ilimchunguza Trump kuhusiana na Urusi'
Kim Jong-un asafiri kwa treni kukutana na Trump
Trump; sihusiki na makosa ya Cohen
Hatahivyo, Cohen ameshtakiwa kwa kulidnagnya bunge alipotoa ushahidi mnamo 2017 kwambajitihada za kujenga jengo refu la Trump huko Moscow zilisitishwa kufikia Januari 2016.

tangu hapo amekiri kwamba kumekuwepo majadiliano yalioendelea hadi Juni 2016 wakati wa kampeni ya uchaguzi, licha ya kwamba ujenzi wa mradi huo haukuendelea.

Cohen ameomba msamaha kwa kauli yake ya awali bungeni, ambayo anatuhumu kwamba 'ilikaguliwa na kuhaririwa' na mawakili wa Trump.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad