Wambura anakabiliwa na mashtaka 17 ambayo anadaiwa kuyatenda katika ofisi za TFF, kati ya Julai mwaka 2004 na mwaka 2015
Inadaiwa kuwa Julai 7, mwaka 2004, Wambura alighushi barua akaiwasilisha TFF akijifanya barua hiyo imeandikwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jek System Limited ikidai malipo ya mkopo wa Dola za Marekani 30,000 zilizokopwa na TFF pamoja na riba.
Wambura anadaiwa alijipatia fedha hizo kwa nyakati tofauti na anashtakiwa kwa mashtaka mawili ya kutakatisha fedha ambapo, kati ya Agosti 15 na Oktoba 24 alitakatisha Sh 25,050,000 na 75,945,024 huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kughushi.