Wanasayansi Wagundua Jipya Kuhusu Bangi


Utafiti uliofanywa na wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani umebaini kuwa uvutaji wa bangi unaongeza nguvu za kiume, kwa yule aliyeitumia hata mara moja tu.


Utafiti huo ambao ulifanywa  kwa wanaume 600, kati ya wanandoa waliohudhuria kliniki ya uzazi, ulibaini kuwa wanaume wanaotumia bangi walikuwa na kiwango cha juu cha uzazi, ikilinganishwa na wasiotumia, kwani utumiaji wa mmea huo unaongeza homoni za kiume ziitwazo Testosterone, ambayo pia humfanya mtumiaji kuwa tayari zaidi kufanya kitu cha kuhatarisha maisha.

Mtafiti Mkuu, Dkt Jorge Chavarro amesema kuwa matokeo haya ambayo hakutarajia yanadokeza kuhusu mambo ambayo hatukufahamu kuhusu umuhimu wa bangi katika suala la uzazi, ama faida zoke kwa jumla, na hata hivyo wanasayansi hao wamesema kuwa utafiti zaidi unahitajika, ili kubaini faida zingine za bangi kwenye afya ya binadamu.

Katika utafiti huu, wanasayansi walikusanya sampuli 1,143 za manii kutoka kwa wanaume 662 katika kipindi cha 2000 na 2017, na uchunguzi wa sampuli za manii ulionyesha kuwa wanaume waliokuwa wamevuta bangi walikuwa na kiwango cha manii cha milioni 62.7 kwa kadri kwa kila milimita, ilhali wale ambao hawajawahi kuvuta walikuwa na milioni 45.4. Ni asilimia 5 tu ya watumiaji wa bangi ambao kiwango chao cha manii kilikuwa chini ya milioni 15, ambacho ndicho kiwango cha kawaida kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)

Ikumbukwe kwamba mmea huo ambao hapa nchini hauruhusiwi kutumika kisheria, umekuwa ukizidi kuhalalishwa siku hadi kwenye nchi zingine za bara la Amerika na Asia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad