“Wanawake Lazima Tuwape Heshima Wanaume”- Rosa Ree

“Wanawake Lazima Tuwape Heshima Wanaume”- Rosa Ree
Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kuchana Rosary Robert maarufu kama Rosa Ree amefunguka na kusema kuwa ni vizuri kama Wanawake watawapa heshima wanaume.

Rosa Ree ameibuka na kusema kwamba ni vizuri Sana  kama Wanawake Wataanza kuwapa heshima wanaume heshima wanayostahili hasa kwa sababu ya mambo mengi ambayo wanayowafanyia.


Katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Rosa Ree amefunguka haya kuhusu heshima kwa wanaume:

Kiukweli inabidi tuwape heshima wanaume, wanajitahidi sana kutufanya tuwe na furaha sio kila siku kuwaimbia wanawake tu kwenye mapenzi, wanaume wanafanya mengi sana kwa ajili yetu ndio maana nimeandika wimbo huu kwa ajili yao”.

Rosa Ree ametoa Wimbo Wake Mpya wa ‘Asante Baba’ ambao ndani yake una ujumbe wa kushukuru wanaume.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad