Wapinzani Waibuka na Sakata la Korosho

Wapinzani Waibuka na Sakata la Korosho
Kambi rasmi ya upinzani bungeni imeishauri serikali kutowabagua wakulima wa korosho kwa kuwalipa wakulima wote pesa zao ili kuwaokoa wanafunzi walioshindwa kuanza shule pamoja na kulipa mikopo.

Hayo yamesemwa na Waziri Kivuli wa Kilimo ambaye pia ni mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari jijini Dodoma.

Mh. Haonga amesema serikali inatakiwa kuacha kuwabagua wakulima wa korosho pamoja na kutakiwa kuzilipa ushuru halmashauri zote ambazo zina wakulima wa korosho ambao asilimia kubwa zinategemea ushuru kupitia zao hilo.

Haonga ameitaka serikali iwe inaanzisha haraka minada ya zao la korosho ili kuepusha uuzaji holela wa zao hilo ambalo katika siku za hivi karibuni soko lake limekuwa likisuasua.

"Mwenendo wa kununua zao la korosho unakatisha tamaaa wakulima na wafanyabiashara kwa ujumla kwani kwani wakati mwingine wanatakiwa waonyeshe mashamba yao ndipo walipwe fedha zao," alisema

Haonga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbozi mkoa wa Songwe alisema kuwa iwapo serikali itaanzisha mapema minada ya korosho, itawapa ahueni wakulima wa zao hilo.

"Ikiwa minada itaanza mapema walau mwezi wa nane badala ya mwezi wa kumi mwishoni utaepusha uuzaji holela kwa kuwa kuna maeneo kama vile wilaya ya Lulindi, Nachunyu na Mvuleni ambapo maeneo hayo korosho zinakuwa tayari zimekomaa," alisema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad