Warioba ashtua viongozi maisha baada ya madaraka

Warioba ashtua viongozi maisha baada ya madaraka
Waziri Mkuu Mstaafu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Rasimu ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba amewashauri  viongozi na wanasiasa vijana waliopo madarakani kuwa na maadili katika kazi zao na kwamba wakumbuke kuna maisha baada ya uongozi.

Jaji warioba ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalumu na www.eatv.tv ambapo amesema kwamba wakati wa kupumzika kama mstaafu unapaswa kupumzika ukiwa na amani ya moyo.

Jaji Warioba ameeleza kwamba yeye wakati alipokuwa kazini alikuwa na ushirikiano na wananchi lakini alipotoka madarakani ndipo aliposhuhudia namna gani wananchi walivyokuwa wakimuheshimu jambo ambalo linamfariji kwa sasa akiwa kwenye mapumziko yake.

Amesema kwamba ili vijana wa sasa waweze kupata heshima ambayo yeye anapatiwa na watanzania, wanapaswa kuwatumikia wananchi kwa moyo mmoja bila kuwa na makandokando yoyote na siyo kuangalia sifa wanazopewa kwa sasa wakiwa kwenye uongozi.

"Nachowashauri vijana waliopo kwenye uongozi, wawatumikie wananchi kwa moyo mmoja. Wanapotoka madarakani wakumbuke kuna maisha mengine yataendelea. Mimi ninafurahi heshima wanayonipa watanzania kwa sasa. Hakuna kitu kizuri kama kuwa na amani ya moyo wakati ukishakuwa umestaafu", amesema mzee Warioba.

"Kwa sasa wakiwa viongozi wanaweza kuwa wanasifiwa lakini ukipewa heshima ukiwa umestaafu ni nzuri kwakuwa tayari unakuwa kwenye maisha mengine," ameongeza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad