Wasanii wa Bongo Fleva wamlilia Godzilla
0
February 13, 2019
Mapema alfajiri ya leo msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Godzilla amefariki dunia ghafla akiwa nyumbani kwao Salasala Dar es Salaam.
Msanii huyo aliyejizoelea umaarufu mkubwa na nyimbo zake Sala Sala, King Zilla, Nataka na nyinginezo kibao.
Wasanii mbalimbali wameonyesha kuguswa na kifo chake, kupitia mitandao ya kijamii wameeleza hisia zao kuhusu kifo cha msani mwenzao.
Mwasiti: Ooh GOD umetangulia zizi jamani!.....niko kwenye maumivu makali mno! MWENYEZI MUNGU ????naomba akupumzishe kwa amani kwenye nyumba yako ya milele.
Fid Q: Inna lillah wainna ilaih raajiuun.. Rest well YOUNG KING!! Kingzilla_tz.
Lulu Diva: Zilla Wewe Jamani Huwezi kunifanyia hivii???????? Daaah jamani Innalilah wainna lillah Rajiun.
Niite Songa: Mungu akulaze pema King Zillah (Golden Jacob), kama alivyo samaki nna mengi ya kusema ila mdomo una maji. Umetuachia huzuni kubwa.
Kala Jeremiah: pUMZIKA KWA AMANI NDUGU YANGU HAKIKA UMETUACHIA MAUMIVU MAKALI. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
R.I.P KING ZILLA.
Vanessa Mdee: Rest Easy King 👑 Happy we lived to witness your greatness. May your legacy live on Baba Shawn @kingzilla_tz.
Dully Sykes: NASIKITIKA KUPATA TAARIFA ZA MSIBA WA MDOGO WANGU GODZILLA NA @missbellatz AMENIPATIA TAARIFA IZO KUA SAA TISA USIKU HUU DOGO KATUTOKA PALE LUGALO HOSPITAL .....R.I.P KING ZILLA.
Lady Jaydee: Hatukumtupa tulijaribu kuwa karibu nae, na kumbe ndio lilikuwa tabasamu la mwisho, we had good time. Rest Easy young bro @kingzilla_tz. Ni ngumu sana kuelewa, ngumu sana kukubali ila kazi ya Mola haina makosa, Tutamkumbuka daima.
Nisha: Natetemeka Zilla wangu dah, daima ulikuwa ukiniita best comedian wako,hata nikinuna unasema nakuchekesha,Zilla umeniweza.
Washkaji zangu nyote mnaondoka dah PUMZIKA KWA AMANI Zilla wangu,M'MUNGU AKUSAMEHE MADHAMBI YAKO msomi wangu msalimie Pancho na King Majuto wangu ðŸ˜.
Mrisho Mpoto: Godzilla naongea na wewe kama bado upo Hai ndugu yangu...nimepokea kwa masikitiko makubwa sana kuondoka kwako, nimeumizwa na msiba wako King King Mungu aipumzishe roho yako King,umetuachia somo kubwa la upendo na kupendana na kukataa makundi ya yakubaguana na kujengeana chuki R.I.P @kingzilla_tz
Tags