Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako amewasimamisha kazi watumishi sita wa chuo cha elimu maalum Patandi mkoani Arusha kwa tuhuma za kushindwa kusimamia majukumu yao na pia matumizi mabaya ya zaidi ya bilioni 2.3 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho.
Waziri Ndalichako amechukua hatua hiyo baada ya kutembelea chuo hicho kukagua mradi wa majengo ya chuo hicho ambao licha taarifa kuonyesha kuwa umechelewa kukamilika bila sababu za msingi pia thamani ya fedha zinazotajwa inapingana na hali halisi na pia ubora wake,na amemuagiza Katibu mkuu kupeleka watendaji wengine wakati uchunguzi ukiendelea na ikithibitika sherika itachukua mkondo wake.
Watumishi waliosimamishwa ni mhasibu mkuu, Rose Kijaka; makamu mkuu wa chuo, Isack Myovela; mwenyekiti wa kamati ya mapokezi, Peter Mosha; boharia wa chuo, Charles Njarabi; na Henry Matei aliyehamishiwa Chuo cha Ualimu Monduli ambaye ameagiza arudishwe kujibu tuhuma zinazowakabili.
Kuhusu mkuu wa chuo hicho, Janes Liana amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo, kumuondolea madaraka na kuendelea na utumishi kutokana na maradhi yanayomsumbua kwa muda mrefu.
Watumishi sita chuo cha elimu maalum Patandi wasimamishwa kazi Arusha kwa tuhuma za ubadhirifu.
0
February 04, 2019
Tags