Kwa niaba ya serikali Waziri Mkuu amesema kuwa Ruge alikuwa mwenye mchango mkubwa sana ndani ya serikali na taifa kwa ujumla.
"Marehemu ndani ya Serikali amefanya kazi kubwa sana kwa kutafsiri philisophia ya viongozi wetu. Alianza awamu ya Nne (chini Rais Mstaafu Dkt Kikwete) na awamu hii ya tano...Amefanya kazi kubwa ya kuelimisha, ametoa mchango mkubwa wakati mwingine hata wa fedha zake." Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Ameendelea kwa kusema, 'Kwa niaba ya Serikali, kwa niaba ya Rais Dkt Magufuli ambaye anaendelea na itifaki zake lakini atakuja, nimekuja kutoa salamu za awali,'.
Ruge Mutahaba amefariki siku ya jana nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo. Ruge alizaliwa mwaka 1970, Brooklyn nchini Marekani, atakumbukwa zaidi kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya muziki nchini.