Bodi ya Filamu Tanzania imetangaza leo kumfungulia muigizaji Wema Sepetu baada ya adhabu ambayo ilitokana na video yake ya kimahaba kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Akitoa uamuzi huo mbele ya vyombo vya habari, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Joyce Fissoo amesema kuwa Wema amefuata maelekezo aliyopewa na bodi hiyo kwa asilimia 75.
“Hatujamfungulia sababu ya huruma, tumemfumngulia sababu amefanya tuliyoagiza kwa zaidi ya asilimia 75”, amesema Fissoo.
Oktoba 26, 2018 Bodi ya Filamu nchini, ilimfungia muigizaji maarufu wa filamu mwanadada, Wema Sepetu kutojishughulisha na uigizaji kwa muda usiojulikana, kufuatia picha zake chafu zilizosambaa mtandaoni.
Kabla ya kufungiwa Oktoba 25 Wema aliomba msamaha kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea siku kadhaa nyuma ambapo ilimuonesha akiwa faragha na mwanaume anayesemekana ni raia wa Burundi, aliyedai kuwa ni mume wake mtarajiwa.
Wakati yote yakijiri mwanadada huyo anatuhumiwa kusambaza picha za ngono kupitia mtandao wake wa kijamiii ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 21, 2019 kumsomea maelezo ya awali.