Zahera azungumzia kipigo cha bao 10 cha Simba

Zahera azungumzia kipigo cha bao 10 cha Simba
Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, raia wa DR Congo, Mwinyi Zahera ametupa dongo jipya kwa timu ya Simba kufuatia kichapo cha mechi mbili mfululizo za Klabu Bingwa Afrika kwa jumla ya mabao 10-0.

Ameyasema hayo wakati timu ya Yanga ilipowasili mjini Babati kwa mapumziko mafupi kabla ya kuelekea Singida ambako inatarajia kucheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya wenyeji Singida United hapo kesho.

Zahera amesema, "mpira ni sheria, ukifuata sheria tu kila kitu kinakuwa sawa, hata sisi tungekuwa na pointi nyingi sana. Sisi tunafanya kazi yetu kama inavyotakiwa na wachezaji pia wanatimiza majukumu yao vizuri lakini kuna watu ndio wanharibu mpira", amesema Zahera.

"Vitu kama hivyo haviwezi kuendeleza mpira wetu bali vinarudisha nyuma, na ndiyo maana nyinyi wenyewe mnaona timu inatoka nje inapigwa mabao 10 sababu gani, sababu ni hiyo", ameongeza.

Klabu ya Simba imepoteza mechi zake mbili mfululizo za mwisho za Klabu Bingwa Afrika ambazo amecheza ugenini, ambapo katika mchezo dhidi ya AS Vita Club ilifungwa maba0 5-0 mjini Kinshasa na mchezo wa wikiendi iliyopita, ilifungwa na Al Ahly ya Misri kwa idadi hiyohiyo ya magoli mjini Alexandria.

Katika hatua nyingine, Yanga ikiwa mjini Babati wakiongozwa na kocha wao mzambia, Mwinyi Zahera walikarimiwa na mashabiki kwa kupatiwa chakula cha jioni,  mafuta ya gari lita 100 na maji katoni 10 katika kuwaunga mkono ili waweze kufanya vizuri katika mechi hiyo itakayochezwa jumatano.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad