Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe yupo nchini Ujerumani kuhudhuria Mkutano Mkuu wa chama cha Die Linke. Mkutano Mkuu huo utafanyika kuanzia tarehe 22 Februari 2019 mpaka 24 Februari 2019 mjini Bonn, Ujerumani.
Zitto Kabwe kushoto
Katika safari hiyo Ndugu Zitto ameambatana na Ndugu John Patrick Mbozu, Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Ndugu Mwanaisha Zuberi Mndeme ambaye ni Katibu wa Ngome ya Wanawake.
Kabla ya Mkutano huo, Ndugu Zitto atafanya mazungumzo na asasi za kiraia leo mjini Berlin, kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea Afrika hususani Tanzania.
Kiongozi wa chama atapata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa European Left Ndugu Gregor Gysi. Baada ya hapo Ndugu Zitto atakutana na Mbunge wa Die Linke katika Bunge la Ujerumani Ndugu Eva Maria Schreiber ambaye ni mjumbe wake mwenza katika programu ya “Mbunge amlinde Mbunge”.
Zitto Kabwe atinga Ujerumani, kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu Tanzania
0
February 21, 2019
Tags