Abiria mmoja wa ndege nchini China, amepigwa faini ya Euro 5,600 sawa na Tsh milioni 15 za Kitanzania kwa kosa la kurusha sarafu kwenye injini ya ndege ya abiria.
The man tossed two coins towards a plane operated by China's Shenzhen Airlines (file photo)
Abiria huyo aliyetambulika kwa jina la Li, alirusha sarafu mbili (2 Coins) wakati akiwa kwenye ngazi akipanda ndege hiyo, ya shirika la ndege la Shenzhen Airlines linalofanya kazi za usafirishaji nchini humo.
He wanted to pray for a safe flight after being inspired by a conversation he had had with other people at the boarding area.
Li, alipopelekwa mahakamani mjini kujibu kesi yake ya kusababisha kuchelewa kwa safari na kuzua taharuki, amesema alifanya hivyo kujaribu shabaha yake na hakujua kama lilikuwa ni kosa.
Abiria wenzake ndio waliomuona na kwenda kuripoti kwa wahudumu, ambapo shirika hilo limeeleza kuwa kitendo hicho kilipelekea kuingiza hasara ya Euro 7,000.
Tukio hilo lilitokea mwaka 2017 katika uwanja wa ndege wa Wuhan Tianhe mjini Wuhan na hukumu yake imesomwa Jumatatano ya wiki hii.
Abiria Apigwa Faini ya Milioni 15 kwa Kurusha Sarafu Kwenye Injini ya Ndege,
0
March 15, 2019
Tags