Ahukumiwa Miaka 30 Jela kwa wizi wa kutumia silaha

Ahukumiwa Miaka 30 Jela kwa wizi wa kutumia silaha
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Sande Teu mkazi wa Mtaa wa Mjimpya Kata ya Mpwapwa mjini ambaye ni mdogo wa Mbunge wa zamani wa Mpwapwa, Gregory Teu kwa kupatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha.

Kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Mpwapwa, Pascal Mayumba na kuendeshwa na mwendesha mashitaka wa polisi, Stephen Masawa.

Hakimu Mayumba aliieleza mahakama kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa hilo siku ya Desemba 27, 2018 katika Kijiji cha Vighawe alimshambulia Bwana Meshack kwa kumpiga na vitu vizito kichwani ikiwemo nondo na rungu.

Hivyo kumsababishia majereha na maumivu mwilini mwake ikiwemo kichwani mikononi na miguuni na kumpora pikipiki.

Aidha, Hakimu Mayumba alisema bila halali mtuhumiwa alitenda kosa hilo kinyume na Sheria namba 287 (A) namba 16 ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Pia alisema kesi hiyo iliyopewa nguvu na mashahidi wanane na vielelezo vilivyopelekwa mahakanani bila kuacha shaka yeyote mtuhumiwa alipatikana na hatia.

Katika utetezi wake mtuhuhumiwa alisema mambo yote yaliyozungumzwa mbele yake sio kweli.

Pia aliomba mahamakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana familia ya mke na watoto wanamtegemea.

Mwendesha mashitaka wa polisi, Stephen Masawa aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa kutokana na madhara ya wanayoyapata wahangawa wizi wa kutumia silaha na kuwataka vijana kupenda kufanya kazi kuliko kutegemea vitu vya wizi na utajiri wa haraka haraka.

Hakimu Mayumba aliambia mahakama kuwa,mtuhumiwa atafungwa kifungo cha miaka 30 jela kutokana na kupatikana na hatia na kutokana na ushahidi na vielelezo vilivyo wasilishwa mahakanani.

Alisema kwa yeyote ambaye hajaridhishwa na hukumu hiyo ana haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad