Alichokisema Mtoto Wa Lowassa, Fred Lowassa Wakati wa Mapokezi ya Baba Yake Arusha

Alichokisema Mtoto Wa Lowassa, Fred Lowassa Wakati wa Mapokezi ya Baba Yake Arusha
Mamia ya wakazi wa Arusha wamekusanyika uwanja mdogo wa Arusha kumsubiri Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lowassa aliyetimkia Chadema akitokea CCM ambako alipitishwa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Mei mosi, 2019 alitangaza kurudi CCM na leo Jumamosi Mei 9, 2019 anarejea nyumbani kwake, Monduli mkoani Arusha.

Watu hao wakiwepo familia ya Lowassa, wakiongozwa na mtoto wake, Fred Lowassa wamesema wamerejea nyumbani CCM na Lowassa.

Fred ambaye naye alijiunga na Chadema baada ya baba yake kutimkia Chadema Julai 28, 2015, amesema familia yote ya Lowassa imerejea nyumbani CCM.

"Kama alivyosema mzee amerudi nyumbani na sisi kama familia tumerudi kumuunga mkono" amesema Fred leo Jumamosi Machi 9, 2019 jijini Arusha.

Amesema anajisikia vizuri kurudi nyumbani kuendelea kushirikiana na rafiki zake ambao aliwaacha CCM na ambao bado wapo Chadema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad