Askari Magereza Wasimamishwa Kazi Kisa Wafungwa Kumiliki Simu Gerezani

Askari Magereza Wasimamishwa Kazi Kisa Wafungwa Kumiliki Simu Gerezani
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Massauni amemuagiza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini kuwasimamisha kazi Askari wanne wa Jeshi la Magereza katika Gereza kuu la Ruanda Mbeya baada ya kubaini wafungwa wa gereza hilo kumiliki simu na kutumia madawa ya kulevya wakiwa grezani.

Hamad  Masauni amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo na kuzungumza na wafungwa pamoja na kufanya ukaguzi ulioonesha kuwa simu hizo zinatumika kwa kufanya vitendo vya rushwa kwa kutumiana miamala ya kifedha baina ya wafungwa au ndugu wa wafungwa na askari hao.

Kufuatia ukiukwaji huo wa taratibu, Naibu Waziri Masauni amemuelekeza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini kuwasimamisha kazi Askari wanne ambao wamebainika kutumia  simu hizo  za wafungwa kupitia miamala ya kifedha ambayo imeonekana baada ya simu hizo kuchunguzwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila  amesema pamoja na hatua ambazo zimechukuliwa na Naibu Waziri Masauni,  bado ipo haja ya Mkuu wa Gereza la Ruanda  kujitathmini kama bado anastahili kuendelea na nyadhifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad