Baba mzazi wa Ephraim Kibonde afunguka baada ya mwanae kufariki

Baba mzazi wa Ephraim Kibonde afunguka baada ya mwanae kufariki
Baba mzazi wa aliyekuwa mfanyakazi wa Clouds FM Ephraim Kibonde amezungumzia kuhusu kifo cha mtoto wake na kusema kuwa ni mtoto wa pili katika familia na amezaliwa mwaka 1972 Upanga jijini Dar es Salaam.

Vilevile amesema kuwa Ephaim Kibonde amesoma hapa Dar es Salam na ameacha watoto watatu ambao ni Junior, Hilda na Illaria.

Mapema leo Mtangazaji huyo amefariki akiwa Mwanza, baada ya kusumbuliwa na Presha toka Bukoba kwenye msiba wa Ruge Mutahaba na kuhamishiwa Mwanza. Kifo cha mtangazaji huyo kinakuja siku chache baada kufariki Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media,Ruge Mutahaba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad