Balozi wa Ujerumani apewa saa 48 kuondoka Venezuela

Balozi wa Ujerumani apewa saa 48 kuondoka Venezuela
Venezuela imemfukuza nchini mwake balozi wa Ujerumani Daniel Kriener, hatua iliyokoselewa vikali na mataifa yanayomuunga mkono kiongozi wa upinzani Juan Guaido, huku Marekani ikitangaza vikwazo zaidi kwa Venezuela.

Wizara ya mambo ya nje imempa balozi huyo wa Ujerumani Daniel Kriener masaa ya 48 ya kuondoka nchini humo kwa madai ya kuingilia masuala ya ndani ya Venezuela. Balozi Kriener alionekana uwanja wa ndege wa Caracas akimkaribisha Juan Guaido wakati alipokuwa akirejea nchini humo siku ya Jumatatu.

Guaido amesema hatua ya kufukuzwa kwa Kriemer itachukuliwa kama kitisho dhidi ya ulimwengu huria. Kriener alikuwa miongoni mwa mabalozi wengine waliomkaribisha Guaido, anayetambuliwa na mataifa zaidi ya 50 kama rais wa mpito, lakini ni yeye pekee aliyefukuzwa na ni mtu asiyetakiwa tena nchini humo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas amesema hatua hiyo inayotajwa na wachambuzi wa Venezuela kama ujumbe kwa walio mstari wa mbele kuipinga serikali ya Maduro inazidi kudhoofisha hali ya mambo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad