CRIMINAL Appeal 370 ya mwaka 2018 ya Mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe, Bob Chacha Wangwe, imesomewa hukumu ya kesi yake asubuhi ya leo majira ya saa tano mchana.
Wangwe ameshinda kesi dhidi ya Jamhuri leo Jumatano, Machi 27, 2019 baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuiona hukumu ya awali dhidi yake haikuwa na mashiko.
Wangwe alishtakiwa na Jamhuri na kukutwa na hatia na Mahakama ya Kisutu kwa kusambaza ujumbe uliodaiwa kwenda kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.
Novemba 15, 2017 alihukumiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa faini ya Sh 5,000,000 au kifungo cha mwaka mmoja jela.
Hata hivyo, hakuridhika na maamuzi hayo ingawa alilipa faini hiyo na kuendelea kuwa uraiani kabla ya kuamua kuikatia rufaa hukumu hiyo.