Bunge la Uingereza Lapiga Kura ya Makubaliano ya Kujiondoa EU

BUNGE la Uingereza jana (Ijumaa) lilimepiga kura  kupitisha sehemu ya makubaliano kwa taifa hilo kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya (EU).



Kura hiyo ilihusu tu makubaliano ya Uingereza kujiondoa, na si tamko tofauti la kisiasa kuhusu mahusiano na hali ya baadaye kati ya nchi hiyo na EU.



Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, anafanya jitihada za dakika za mwisho kuwashawishi wabunge kupitisha makubaliano hayo aliyofikia na EU, lakini wataalam wanasema anakabiliwa na uwezekano wa kushindwa kwa mara nyingine.



Hapo awali,  siku ya ijumaa ndiyo ilikuwa imepangwa Uingereza kujiondoa rasmi kwenye umoja huo. Hatua ya Uingereza kujiondoa EU ilikumbwa na changamoto nyingi  Jumatano iliyopita kuliko ilivyokuwa awali, baada ya bunge kukataa mapendekezo mbadala manane ya Theresa May.



EU ilikuwa imekubali kusogeza mbele tarehe ya Brexit (kujitoa kwa Uingereza katika EU)  hadi Mei 22, iwapo makubaliano ya kujiondoa yataidhinishwa na bunge la Uingereza wiki hii.



Kama hawataidhinisha makubaliano hayo, mchakato wa kujiondoa utarefushwa hadi Aprili 12, ambapo Uingereza itahitajika kutoa mapendekezo jinsi ya kuendelea na mchakato wake wa kujiondoa EU.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad