Kwa mujibu wa habari zilizoifikia meza ya eNewz ya EATV kwamba mke wa msanii wa muziki wa Dansi kutoka bend yaTwanga Pepeta,Charz Baba aliyemuoa mwishoni mwa mwaka jana alikuwa ni mpenzi wa msanii wa bongo fleva Ali Kiba.
Imefahamikwa kwamba mwanadada huyo huenda angeolewa na Alikiba endapo asingekwenda kuoa Mombasa.
Charz amesema hajui chochote kuhusu mahusiano ya Ali Kiba na mke wake na anachokijua yeye ni kwamba mke wake na familia ya Kiba zina ukaribu na ndio maana hata katika harusi ya mdogo wake Ali, Zabibu Kiba, mwanadada huyo alikuwa mtu wa karibu sana katika kukamilisha harusi hiyo.
"Nimeamua kufunika kombe ili mwanaaramu apite na ukitaka kumchunguza bata utashindwa kumla utaishia kutapika,mapenzi yanamambo mengi sana ukitaka kuyafatilia yote huwezi kukaa kwenye ndoa mimi na mke wangu kila mtu anamadhambi yake ila tulikaa chini tukaamua kuachana na ya nyuma na kuanzia familia yetu", amesema Charz
Pia Charz alimalizia kwa kusema kitendo cha Ali Kiba kuja na kuimba kwenye harusi yake hiyo inadhihirisha wazi kwamba roho yake ni nyeupe na hana tatizo lolote na mke wake hivyo kwa sasa wanaishi na mke wake kwa upendo na amani na hakuna kati yao anayeangalia historia ya zamani ya kimapenzi kati yao.