Claudio Ranieri atua rasmia AS Roma

Zikiwa zimepita siku nane tangu atimuliwe Fulham, Claudio Ranieri leo ametangazwa kuwa kocha mpya wa AS Roma akichukua nafasi ya Di Francesco aliyefutwa kazi jana alhamisi.

Ranieri ambaye amewahi kuifundisha Roma kati ya mwaka 2009 na 2011, amepewa kandarasi ya kuiongoza timu hiyo kwa sasa.

Kocha wa zamani wa vilabu vya Leicester and Chelsea, Claudio Ranieri(67) ameteuliwa kuinoa klabu ya AS Roma hadi mwisho wa msimu huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad