Clouds Media Group Bila Ruge Tutarajie nini?

Kwa masikitiko makubwa napenda kutoa pole kwa familia nzima ya Prof Mutahaba,CMG ndugu jamaa na marafiki kwa kumpoteza kijana mahiri,visionary mastermind wa tasnia nzima ya burudani nchini,hakika hakuna anayefurahia kifo cha mwanadamu mwenzake isipokua mchawi na mwanasiasa tu pumzika kwa AMANI RUGE.

Back to the topic,kila.mmoja anajua kwamba taasisi imara ni ile ambayo imejengwa katika misingi ya kutomtegemea mtu bali mfumo,kanuni hii imekua ni kinyume kabisa kwa ndugu zetu hawa wa CMG ambao katika kila sikio la mtanzania ameskia wafanyakazi wa media hiyo wakimtaja Boss Ruge (R.I.P) kama ni genius,Akili kubwa,Chuo Kikuu kwa maana yeye ndio alikua kila kitu pale mjengoni na wengine ni wafata upepo tu,mtihani mdogo walioputa CMG pasi na uwepo wa Ruge ni ule uliopelekea kuahirishwa kwa tamasha la fiesta jambo ambalo tuliwaskia watu wengi wakiwemo wanafamilia wa Clouds wakisema "angekuwepo Ruge wasingefuta Fiesta angepambana hadi kieleweke" Kwangu mimi binafsi ule ni udhaifu mkubwa sana kwa afya ya taasisi,why Ruge? ina maana hakuwatrain watu wengine kujua mbinu alizokua anatumia kufanikisha mambo ya taasisi ile?

Now Ruge has gone  kwa sasa tutegemee majaribu mengi sana kwa chombo hiki cha habari,yatakayopelekea hatari ya kupotea kwenye ramani endapo hawataondoa ile mentality "angekuwepo Ruge" they need to stay strong and focus.....

By Madimba Jr

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad