Msanii wa muzik Bongo, Diamond Platnumz amekutana na aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Cameroon, Samuel Eto'o nchini Ufaransa.
Muimbaji huyo kutokea WCB amechapisha picha kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuisindikizia na ujumbe iliyosomeka;
"Because making Our African Continent Proud is our Pleasure... A blessed day at My brother Samuel Eto'o Paris Home," ameeeleza Diamond.
Pia meneja wa muimbaji huyo na WCB kwa ujumla, Sallam SK amechapicha akiwa na mchezaji huyo aliyepata kuvichezea vilabu vikubwa barani Ulaya kama Barcelona, Inter Milan,Chelsea na viginevyo.