DC Jokate afunguka kuhusu hatima ya bidhaa zake za Kidoti


Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegero ambaye kabla ya kuchaguliwa alikuwa akijihusisha na maswala ya urembo na fasheni amesema ataendeleza chapa ya Kidoti mara baada ya kuimarika kwenye Uongozi.

DC Jokate ameeleza hayo kwenye Mahojiano na kipindi cha The Playlist cha Times FM ambapo amesema nembo ya kidoti haiwezi kufa itarudi wakati wowote

"Unajua ile ni brand ambayo tumeitengeza kwa nguvu nyingi, kwasasa ilikuwa ni kujifunza kuhusu uongozi, nikitulia vizuri nitatafuta timu nzuri ili iweze kubeba wazo langu” Amesema Jokate

Utakumbuka kuwa Jokate alikuwa akitengeeza mabegi ya shule, ndala na nywele zenye chapa ya kidoti kabla ya kusimama alipochaguliwa kuwa mkuu wa wilaya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad