Dudu Baya Aachiwa kwa Dhamana

Dudu Baya Aachiwa kwa Dhamana
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, limemuachia kwa dhamana msanii  Godfrey Tumaini (Dudu Baya) baada ya kumshilikia kwa saa kadhaa.

Dudu Baya alikamatwa juzi Jumatano na polisi na kufunguliwa jalada la kesi lenye namba OB/RB/2029/2019 la matumizi mabaya ya mitandao.

Hatua hiyo ilikuja  baada ya Waziri wa Habari na Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kuagiza Jeshi la Polisi na Baraza la Sanaa la Taifa(Basata) kumchukulia hatua mwanamuziki huyo kwa makosa ya kumdhihaki, aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Ruge Mutahaba kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu amesema walimwachia msanii huyo jana Alhamisi, Februari 28 saa 9:00 mchana baada ya kumaliza kumuhoji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad