FAHAMU: Mambo 8 kuhusu ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines, ikiwemo PICHA za eneo ilipoanguka
0
March 10, 2019
Leo Jumapili Machi 10, 2019 Afrika imepatwa na mshtuko mkubwa baada ya ndege ya shirika la ethiopian Airlines kuanguka nchini Ethiopia majira ya saa 2:38 asubuhi.
Hapa tumekuandalia mambo 8 kuhusu ajali hiyo, ambayo imeacha simanzi barani Afrika.
1- Ndege ilikuwa na Abiria 147 na Wahudumu nane na wote wamefariki dunia hakuna aliyetoka hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Shirika hilo, Tewolde Gebremariam.
2-Ndege hiyo aina ya Boeing 737 MAX ET302. Ilipoteza mawasiliano dakika 6 baada ya kuruka kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, uliopo Jijini Addis Ababa, Ethiopia.
3- Abiria na wafanyakazi waliokuwemo kwenye ndege, wanatoka katika mataifa 33 tofauti tofauti.
4-Hii ni ajali ya kwanza kubwa ya ndege kutokea nchini Ethiopia tangu Waziri Mkuu wa Taifa hilo, Abiy Ahmed aingie madarakani na ndiye mtu wa kwanza kutoa taarifa hizo za ajali.
5-Ndege hiyo imeanguka katika eneo la kusini mashariki mwa Addis Ababa karibu na mji wa Bishoftu. Inakadiriwa kuwa ni kilometa 60 kutoka katika uwanja wa ndege wa Bole.
6-Toleo lingine la ndege linalofanana na ndege hiyo, lilipata ajali kama hiyo miezi mitano iliyopita huko Indonesia ambapo ndege ilikuwa mali ya Shirika la Lion Air na watu wote 190 walifariki dunia.
7-Nchi zilizoongoza kuwa na abiria wengi kwenye ndege hiyo ni Kenya (32) ikifuatiwa na Canada 18. #Updates
8-Toleo la Boeing 737 MAX ndio toleo jipya na pendwa zaidi, kwani ndio limeongoza kwa mauzo mpaka sasa.