Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe jana March 27, 2019 ameongoza kikao cha viongozi wa vyama 10 vya upinzani nchini na wanasiasa waandamizi .
Kikao hicho kilifanyika saa chache baada ya polisi kuzuia mkutano wa ACT uliokuwa ufanyike ukumbi wa PR Temeke kwa kile kilichoelezwa kuwa wamepata taarifa kuwa kuna wanachama wa CUF ambao walitaka kufanya vurugu.
Mmoja wa watu walioudhuria kikao hicho alidokeza kuwa kilijadili juu ya vyama hivyo kushirikiana katika nyanja mbalimbali.
“Kikao kilijadili mambo mengi ya kushirikiana, tumejadili suala la Sheria mpya ya Vyama vya Siasa, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika mwaka huu na tisho la kufutwa kwa ACT,” kilidokeza chanzo hicho.
Kilisema ushirikiano huo utaenda mbali zaidi kadiri muda utakavyoenda, yote ikiwa ni kusimamia misingi ya demokrasia.
Freeman Mbowe Aongoza kikao cha viongozi wa vyama 10 vya upinzani Nchini
0
March 28, 2019
Tags