Gari za abiria zapigwa marufuku kusafirisha vifurushi na barua

Gari za abiria zapigwa marufuku kusafirisha vifurushi na barua
Niabu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh Mhandisi Atashista Nditiye amepiga marufuku magari yote ya abiria kusafirisha vifurushi vya aina yoyote zikiwemo barua bila kuwa na leseni ya mamlaka ya mawasiliano nchini, huku akiitaka mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini nan chi kavu SUMATRA kuendesha oparationi kali kudhibiti vitendo hivyo.


Naibu Waziri Nditiye ametoa agizo hilo mjini Musoma mkoani Mara wakati akizungumza na watumishi taasisi mbalimbali ambazo ziko chini ya wizara hiyo ikiwemo kampuni ya simu nchini TTCL na shirika la Posta Tanzania.

Hata hivyo amewataka watendaji wa taasisi hizo kuziendesha taasisi hizo kwa faida, ikiwa ni pamoja na kutumia vema fedha zinatolewa na serikali kuu kama ruzuku,na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa watendaji watakaobainika kwenda kinyume na maelekezo hayo.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. dah,this is tanzania itafika hatua ata ukitumwa mzigo upeleke mahali unatakiwa uwe na leseni kutoka tcra...,kila kukicha matamko tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad