Msanii wa Muziki, Harmonize amefunguka hisia zake kwenye wimbo wake aliwahi kumuweka kama video vixen aliyekuwa Mpenzi wake Wolper na huu mpya aliomuweka mpenzi wake wa sasa Sarah.
Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa hauwezi kufananisha ile video ya kwanza aliyoshoot na naniliu akaweka... Fundi Naniliu ambapo Mpenzi wake wa zamani huyo anajiita fundi cherehani wa kishua.
"Nilikwambia kuwa Baby yupo katika #AfroBongo na ameuwa 😂 tuseme ukweli huwezi fananisha na ile video ya kwanza niliyo shoot na naniliu....!!!! Fundi naniliu 😂😋😋 Natania 😂 ila Mtoto kama sio wewe waliekuwa wanakuita Sarah Masai.....????? Thanks for the Love & support @sarah__tz ❤❤❤❤ OYAAAAA LINK PA BIO," aliandika Harmonize.
Hata hivyo nae Wolper hakukaa kimya amejibu mashambulizi hayo kwa kusema kuwa Mwaka 2019 hatoi kiki huku akisema kuwa video acheze mwingine caption aandikwe mwingine Pazitoo.
Pazitoooooo,Sitoikiki2019 👉💰,sema mapensi mavumilivu sana vdio acheze mwingine caption Andikwe mwingine ,kunimiss kama kotee ," aliandika Wolper.
"Iknow bby But nipo kwenye Dunia yangu kama hivi Naogelea."
Machi 16, 2017, Harmonize alitoa wimbo wake wa 'Niambie' aliomuweka Jacqueline kama video vixen.