Hii Hapa Hoteli ya Kwanza Duniani Katika Anga ya Juu

Hii Hapa Hoteli ya Kwanza  Duniani Katika Anga ya Juu
Ilinuiwa kusisimua safari za duniani: Kituo cha Aurora hoteli ya kwanza duniani - kwenye mzunguko wa obiti katika anga za juu.

Tangazo rasmi kuhus mpango huo lilitolewa Aprili mwaka jana huko San Jose, California Marekani.

Imejengwa kwa ukubwa wa ndege kubwa ya kibinafsi, itakayoruhusu watalii kupaa maili 200 juu ya ardhi ya dunia, na kupata fursa ya kutupia jicho mandhari ya sayari na muanga wa kaskazini na kusini.

Gharama sio nyepesi: safari hiyo ya siku 12 kwenye kituo cha Aurora inayotarajiwa kufanya ziara ya kwanza yakitalii mwaka 2022, ni ya thamani ya $9.5m kwa mtu mmoja.

Hatahivyo, kampuni hiyo inasema orodha ya watu wanaosubiri safari hiyo ya kitalii inakusanywa miezi 7 kabla ya safari yenyewe.


"Sehemu ya hisia tunayotaka kuwapatia watu ni kujua maisha halisi ya mwana anga za juu yalivyo," amesema Frank Bunger, muasisi na mkurugenzi mtendaji wa Orion Span, kampuni inayosimamia uidhinishaji wa hoteli hiyo ya Aurora.

"lakini tunatarajia wageni wengi watakuwa wakichungulia nje ya madirisha , na kuwaita kila wanaowajua, na iwapo watachoka, tuna tunachokita 'holodeck,' mfumo wa uhaisia unaoonyesha hali ilivyo, na unaweza kufanya chochote unachotaka kufanya mfano kuelea katika anga za juu, kutembea kwenye mwezi na hata kucheza gofu."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad