Je, Polisi Anaweza Kukushikilia Mafichoni na Kukuhoji Bila Kukupa Nafasi ya Kuwa na Mwanasheria?


Hapana. Jeshi la Polisi likikushikilia mafichoni ni kinyume cha sheria. Askari Polisi wanapokuweka rumande ni jukumu lao kuangalia afya yako na kuzilinda haki zako

Iwapo utapata madhara yoyote au haki zako hazitaheshimiwa na zikavunjwa kwa namna yoyote ile Jeshi la Polisi litawajibika

Askari Polisi wana wajibu wa kuandika taarifa za watu wote wanaofika kituoni kwenye kitabu chao cha kumbukumbu za kila siku. Kitaonesha muda ulioletwa hapo kituoni kwa mahojiano na wakati gani ulikamatwa

Kumbuka kuwa unayo haki ya kuwa na mwanasheria wako wakati wa kuhojiwa.

Hivyo, sehemu ya mahabusu lazima ijulikane na iweze kufikiwa na mwanasheria wako, marafiki, familia au jamaa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad