Kagame Aeleza Chimbuko la Mgogoro Kati Ya Rwanda na Uganda

Kagame Aeleza Chimbuko la Mgogoro Kati Ya Rwanda na Uganda
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameelezea kuwa chimbuko la mgogoro baina ya nchi yake na nchi ya Uganda ni la tangu miaka 20 iliyopita nchi ya Uganda ikitaka kuangusha utawala wake.

Akihutubia mkutano wa kitaifa Rais Kagame amesema mgogoro huo ulishika kasi mnamo miaka ya hivi karibuni kutokana na serikali ya Uganda kuunga mkono kundi la RNC linalopinga Rwanda na ambalo linatumiwa na Uganda kuwanyanyasa raia wa Rwanda wanaotembelea au wanaoishi nchini Uganda.

Akihutubia mkutano wa kitaifa unaomkutanisha na viongozi wengine kuanzia ngazi ya mashinani,rais Paul Kagame amezungumzia kwa kirefu mgogoro baina ya Rwanda na nchi ya Uganda na kusema mgogoro huo ni wa tangu miaka 20 iliyopita.

Akifafanua mgogoro huo Rais Kagame amerejelea kitabu kinachoitwa 'From Genocied to continental War'' ambacho kiliandikwa na Gerard Prunier mwanishi wa vitabu kutoka Mfaransa.

Rais Kagame amesema kwamba mwandishi huyo aliandika kwamba alikutana na waziri wa zamani wa mambo ya ndani marehemu Seth Sendashonga mwaka 1998 pmaoja na maafisa wakuu wa jeshi la Uganda na kuzungumzia mipango ya kumsaidia Sendashonga ili kuangusha utawala wa Kagame.Mwandishi huyo katika kitabu chake kulingana na maelezo ya rais Kagame, Uganda ilikuwa imemuahidi kumsaidia kijeshi.

''Sababu ya mimi kurejelea kuzungumza haya nimetaka kuwaonyesha mfululizo wa jinsi mambo yalivyokwenda mnamo miaka 20 iliyopita.Tulijaribu kufanya mikutano ya hapa na pale ili kutafuta suluhu.lakini matatizo hayo hayaishi.Ukweli ni kwamba Seth Sendashonga alifariki dunia kwa kuwa alivuka mstari mwekundu.Sifurahii kusema hivyo lakini pia sijutii kifo chake''

Seth Sendashonga aliuawa katika mazingira ya kutatanisha mwaka 1998 mjini Nairobi alipokuwa uhamishoni baada ya kutofautiana na utawala wa Rwanda.

Rais Kagame amesema mgogoro huo ulishika kasi hivi karibuni kufwatia wananchi wa Rwanda wanaoingia nchini Uganda au kufanyia kazi nchini humo kushikwa na kuzuiliwa sehemu ambazo hazijulikani na kufanyiwa vitendo vya mateso huku akishtumu utawala wa Uganda kutoa nafasi ya ushirikiano kwa kundi la Rwanda National Congress linaloongozwa na mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda jenerali Kayumba Nyamwasa:

''RNC wanafanya kazi kwa ushirikiano na vyombo vya usalama vya Uganda.kilicho wazi ni kwamba Wanachokifanya ni kunyanyasa wanyarwanda ambao hawataki kuungana nao huku wakiwasingizia  kwamba wametumwa na utawala wa Kigali kuhujumu usalama wa Uganda na kuuwa wanyarwanda wa upinzani.Ni madai yasiyo na msingi,lakini haya yote yanaonyesha ushirikiano wa dhati uliyopo baina ya serikali ya Uganda na kundi la RNC.''

Uganda imekuwa ikiishutumu Rwanda kuwatuma majasusi na kufanyia vitendo vya ujasusi kwenye ardhi yake,shutuma ambazo Rwanda inakanusha.

Rais Kagame amesisitiza kwamba mara kadhaa mwenyewe aliwasilisha malalamiko hayo kwa mwenzake Yoweri Museveni na kwamba hakuonyesha utashi wowote wa kuyatatua.

Wiki iliyopita serikali ya Rwanda ilikataza wananchi wake kwenda nchini Uganda na kusababisha mkwamo wa biashara.Rwanda inasema inatoa kipaumbele kwa maiasha ya raia wake zaidi kuliko biashara baina ya nchi mbili

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad