Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ashutumiwa Kuikingia Kifua Boeing

Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ashutumiwa Kuikingia Kifua Boeing
Mkaguzi mkuu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon ameanzisha uchunguzi rasmi kuhusiana na shutuma zilizotolewa na asasi moja, kwamba kaimu Waziri wa Ulinzi wa Marekani Patrick Shanahan alitumia cheo chake kuipigia debe kampuni ya Boeing ambayo ni mwajiri wake wa zamani.

Asasi hiyo, Citizens Responsibility and Ethics, ilifungua shauri la kimaadili wiki iliyopita, ikidai kwamba Shanahan ametoa kauli zinazoonekana kuitangaza Boeing na kuwashambulia washindani wake kama Lockheed Martin.

Haya yanajiri wakati kampuni hiyo ikikumbwa na mkasa wa ndege yake chapa Boeing 737 Max 8 ambayo imepata ajali mara mbili katika muda wa miezi mitano, na kuangamiza maisha ya mamia ya watu.

Boeing imesema imetengeneza programu mpya ya kompyuta ya kuendesha ndege hiyo, mbadala kwa iliyokuwepo ambayo inadhaniwa kuwa chanzo cha ajali hizo.

 Msemaji wa mkaguzi mkuu wa Pentagon amesema Shanahan amekwishaarifiwa kuhusu uchunguzi dhidi yake, na ameikaribisha hatua hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad