Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeeza sababu za kuzuia mkutano wa ndani wa chama cha ACT-Wazalendo uliokuwa ufanyike leo asubuhi katika ukumbi wa PR, Temeke jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema wameuzuia baada ya kufanya uchunguzi na kubaini viashiria vya kutokea vurugu katika mkutano huo.
“Mkutano wa ndani hauhitaji maombi ya kibali, ila shida kipindi hiki cha mpito hivi vyama vya ACT na CUF kumekuwa na uhasama wa chini kwa chini, tumepata taarifa watu wa CUF walikuwa wamejipanga kufanya vurugu pale.“ameeleza Mambosasa.
Kamanda Mambosasa alipoulizwa kwanini Jeshi lisingelinda mkutano huo badala ya kuzuia, amesema kuwa Jeshi hilo lilikuwa na majukumu mengine.
Kamanda Mambosasa Afunguka Sababu za Polisi Kuzuia Mkutano wa ACT Wazalendo, CUF Watajwa
0
March 27, 2019
Tags