Kamati ya Fitna Simba Yamaliza Kazi Algeria

Kamati ya Fitna Simba Yamaliza Kazi Algeria
MTENDAJI Mkuu wa Simba, Crecentius Magori, amefunguka kuwa kamati iliyotumwa kuweka mambo sawa nchini Algeria, imekamilisha mipango na kilichobaki ni Simba kushuka uwanjani Jumamosi kufanya mambo.

Magori Alisema waliwatuma wawakilishi wawili kwenda Algeria mapema kwa lengo la kuweka mambo sawa, kubwa ikiwa ni kuunda mipango itakayoifanya Simba ivune pointi kwenye mchezo huo dhidi ya JS Saoura.

“Tulitanguliza watu mapema kule Algeria ili waandae mazingira mazuri, kitu kizuri ni kwamba ripoti waliyotuma inaonesha kuwa mambo ni shwari na suala la kupata pointi ni kubwa sana,” alisema Magori ambaye amewahi kuwa Makamu wa Rais wa TFF.

Katika hatua nyingine, beki kisiki wa Simba, Pascal Wawa amesema; “Ligi ya Mabingwa Afrika ni michuano tofauti kabisa na hii ligi tunayocheza, watu wasifi kiri kuwa mchezo utakuwa mwepesi na tutapata pointi tatu kirahisi kama tunavyofanya kwenye ligi yetu.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad