kapombe Yupofiti Arejea Rasmi Uwanjani

kapombe Yupofiti Arejea Rasmi Uwanjani
BAADA ya kuwa nje tangu Novemba mwaka jana, beki wa Simba, Shomary Kapombe sasa yuko fi ti na anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi wiki ijayo.

 Kapombe aliumia kifundo cha mguu kwenye kambi ya Taifa Stars iliyowekwa nchini Afrika Kusini ambako walikuwa wakijiandaa na mechi dhidi ya Lesotho, beki huyo alifanyiwa upasuaji.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kapombe alisema amefanyiwa vipimo na wamebaini kwa sasa yupo vizuri na ameanza mazoezi mepesi.

“Nilienda Afrika Kusini kufanyiwa vipimo ili kujua maendeleo yangu yako vipi, kwa sasa vipimo vinaonyesha nipo vizuri na nimerejea nchini na sasa kuwa mazuri nitaungana na timu kuanza mazoezi lakini kwa sasa
namshukuru Mungu niko fi ti kiafya,” alisema Kapombe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad